

Description
Dani na Matope Mwilini 1b (Access) ni hadithi ya pili katika msururu wa vitabu vya Dani, iliyoundwa kwa ustadi ili kuendana na Mtaala wa Chekechea (CBC). Hadithi inafuata matukio ya Dani, Galu, na Menza wanapocheza kibe, ambapo Dani anaanguka katika matope. Kitabu hiki kinasaidia watoto kujifunza stadi za kusoma, kufikiri, kuelewa hadithi, na kukuza ubunifu, huku pia kikiwajengea mwanafunzi uwezo wa kujitegemea na kujiamini. Kitabu kinaendana kikamilifu na mtaala wa chekechea na kimeandikwa ili kufanya mchakato wa kujifunza kuwa wa kufurahisha, wa kuvutia, na unaohusisha watoto kwa vitendo. Kitabu hiki kimeandaliwa kwa mtindo unaomshirikisha mwanafunzi kikamilifu kupitia sehemu mbalimbali za kujifunza. Sehemu ya Ahadi Yangu humwezesha mwanafunzi kufanya ahadi ya kusoma kitabu na kujenga nidhamu ya usomaji. Kupitia Sehemu ya Kufanya Utabiri, mwanafunzi huhamasishwa kutabiri kuhusu hadithi kwa kutumia jina la kitabu, picha ya jalada, na vielelezo vilivyomo ndani ya kitabu. Maswali yaliyoandaliwa kwa lugha nyepesi humwongoza mwanafunzi kuelewa vipengele muhimu vya hadithi. Sehemu ya Maoni Yangu humpa mwanafunzi nafasi ya kueleza kama amekipenda kitabu na kilichomvutia zaidi, huku Sehemu ya Mradi Wangu ikimpa fursa ya kufanya shughuli zinazokuza ubunifu, kujitegemea, na kujiamini.
Book details
- Format
- Paperback
- ISBN
- 9789914729238
- SKU
- 9789914729238
- Delivery type
- physical
- Publisher
- Access Publishers
- Language
- Kiswahili
Shipping & returns
Delivery methods, digital access, taxes, and return eligibility are confirmed during checkout for the selected edition and destination.
Book information
Dani na Matope Mwillini
Pauline Kea
- Author:
- Pauline Kea
- Language:
- Kiswahili
- Collection:
- The Nairobi Int'l Book Fair Sept 23-27
Paperback
This edition is currently out of stock.






