Skip to main content
Cover of Jipe Moyo
Description

Jipe Moyo, Diwani ya Mashairi ni diwani yenye mkusanyo wa mashairi yaliyotungwa kutokana na masuala katika mitaala ya Kiswahili, kwa Gredi ya Saba, Nane na Tisa. Mashairi haya yametungwa kwa ufundi mkubwa ili kufundisha stadi mbalimbali za maisha, kuburudisha na kukashifu mambo yasiyofaa katika jamii. Mashairi katika diwani hii yanakidhi maudhui katika masuala mbalimbali kwenye mitaala hii pamoja na kuwa yanaangazia kwa kina masuala ibuka yanayowahusu wanafunzi. Masuala hayo yamewasilishwa kwa njia nyepesi zaidi ili kumwezesha mwanafunzi kujifunza na kufaidi ujumbe kwa urahisi. Mbali na hayo, mashairi haya yametungwa kwa lugha nyepesi ili kueleweka moja kwa moja. Maudhui kwenye mashairi haya yako wazi ili ujumbe ueleweke kwa urahisi. Pamoja na hayo, yanafunza mbinu anuwai za lugha, kwa mfano: tashbihi, sitiari, methali, nahau na uradidi. Isitoshe, kila shairi lina maswali yatakayomwongoza mwanafunzi katika kufahamu, kuelewa na kuchambua mashairi ya Kiswahili katika kiwango hiki. Bila shaka, diwani hii ni hazina bora na tunu ambayo itawatia moyo wanafunzi wa kiwango hiki na kuwafanya wapende na kuchangamkia ushairi.

More details
Format
Paperback
ISBN
9789914442908
SKU
9789914442908
Delivery type
physical
Publisher
Oxford University Press East Africa
Language
Swahili
Shipping & returns

Delivery methods, digital access, taxes, and return eligibility are confirmed during checkout for the selected format and destination.

Book information

Jipe Moyo

Oxford University Press East Africa

Language:
Swahili
Collection:
CBE 2027 Book List

Paperback

1

Jipe Moyo

KES 371.00

Print booksDelivery estimate shown at checkout.
ReturnsEligibility confirmed at checkout.