

Description
KJSEA Nguzo ya Kiswahili (Kitabu cha Marudio kwa Gredi ya 7, 8 na 9) kimeandikwa kwa ufundi mkubwa ili kumkuzia mwanafunzi umilisi katika vipengele mbalimbali vya lugha huku kikimtayarisha vilivyo kwa tathmini ya Kenya Junior School Education Assessment (KJSEA). Kitabu hiki kimeshughulikia mada zote katika mtaala wa kiwango cha Junia kwa njia wazi na nyepesi inayomrahisishia mwanafunzi ujifunzaji na hapo hapo kumpa hamu ya kujifunza. Upekee wa kitabu hiki unajitokeza kupitia yafuatayo: Shughuli tangulizi zinazomchochea mwanafunzi kujifunza kwa njia ya kutafiti na kuulizia maswali dhana mbalimbali. Maelezo ya kina kuhusu stadi na vipengele mbalimbali vya lugha kuanzia Gredi ya 7 hadi Gredi ya 9. Mifano kutoka kwenye mazingira ya mwanafunzi ambayo inasaidia kukuza uhalisia na uelewa wa dhana mbalimbali. Vielelezo anuwai vya aina mbalimbali za kusikiliza na kuzungumza, kama vile kuzungumza kwa kupasha habari. Vielelezo anuwai vya aina mbalimbali za kusoma, kama vile kusoma kwa kina. Vielelezo mbalimbali vya aina tofautitofauti za insha, zikiwemo tungo amilifu, kwa mfano barua na shajara. Vifungu vya kuvutia vinavyosaidia kukuza hamu ya ujifunzaji wa sarufi. Mazoezi anuwal yanayomrahisishia mwanafunzi ujifunzaji na kumpa fursa ya kujitathmini. Tathmini za mwisho wa sura ambazo zinamwezesha mwanafunzi kujitathmini huku zikimtayarisha kwa Tathmini Endelevu za Shuleni (SBA) kwa Gredi ya 7 na 8. Majibu kwa tathmini za mwisho wa sura zinazoemwezesha mwanafunzi kupima umilisi wake. Vielelezo vya tathmini ya KJSEA vinavyomsaidia mwanafunzi kujitathmini na kumtayarisha vilivyo kwa KISEA Majibu kwa vielelezo vya tathmini ya KISEA ambayo yanasaidia kupima uelewa na umilisi wa mwanafunzi huku akikuza kujiamini.
More details
- Format
- Paperback
- ISBN
- 9789914969955
- SKU
- 9789914969955
- Delivery type
- physical
- Publisher
- Newton Educational Resources
- Language
- Swahili
Shipping & returns
Delivery methods, digital access, taxes, and return eligibility are confirmed during checkout for the selected format and destination.
Book information
KJSEA Nguzo ya Kiswahili Kitabu cha Marudio Gredi ya 7,8,9
Newton Educational Resources
- Language:
- Swahili
- Collection:
- CBE 2027 Book List
Paperback
KJSEA Nguzo ya Kiswahili Kitabu cha Marudio Gredi ya 7,8,9
KES 1,150.00





